IQNA

Fikra na urithi wa kielimu wa Ayatullahil Udhma Shahidi Sadr wachunguzwa Iraq

13:34 - April 28, 2011
Habari ID: 2113530
Kikao cha nne cha kuchunguza fikra na urithi wa kielimu wa Ayatullahil Udhma Shahidi Sayyid Muhammad Baqir as-Sadr kilifanyika siku ya Jumanne katika kituo cha utamaduni na Uislamu huko katika mkoa wa Diwaniyya nchini Iraq.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wanafikra, wasomi pamoja na wanazuoni mashuhuri wa Iraq Abdul Rahman Alawan, mkuu wa kituo kilichotajwa alitoa hotuba ya ufunguzi na kuzungumzia kwa ufupi historia ya maisha ya Imam Baqid Sadr na kisha wasomi waalikwa walipewa fursa ya kuzungumzia utafitu wao kuhusiana na fikra za kielimu za mwanazuoni huyo mashuhuri wa Kiislamu. 782384
captcha