IQNA

Maonyesho ya kimataifa ya vitabu vya Kiislamu yafunguliwa Kuwait

17:02 - April 30, 2011
Habari ID: 2114576
Maonyesho ya 36 ya kimataifa ya vitabu vya Kiislamu yamefunguliwa nchini Kuwait. Maonyesho hayo yanadhaminiwa na Jumuiya ya Marekebisho ya Kijamii ya Kuwait.
Maonyesho hayo yaliyofunguliwa Alkhamisi iliyopita na Ahmad al-Fahd As-Swabah, Naibu Waziri Mkuu wa Kuwait anayeshughulikia masuala ya kiuchumi yanafanyika chini ya kaulimbiu ya 'Utamaduni wa Familia' na yamepangwa kuendelea hadi Mei 9. Maonyesho hayo yanayashirikisha zaidi ya mashirika 78 ya uchapishaji na usambazaji vitabu kutoka nchi 6 za dunia.
As-Swabah amesema katika ufunguzi wa maonyesho hayo kwamba kuchaguliwa kwa kaulimbiu iliyotajwa kunabainisha juhudi kubwa zinazofanywa na Jumuiya ya Marekabisho ya Kijamii kwa ajili ya kulinda athamani na misingi ya jamii ya Kiislamu nchini Kuwait. Amesema kulindwa kwa utamabulisho wa Kiislamu ni hitajio muhimu katika ulimwengu wa sasa na kwamba maonyesho hayo ni hatua muhimu kuelekea lengo hilo.
Maonyesho hayo ambayo hufanyika kila mwaka yamekuwa yakiandaliwa na jumuiya iliyotajwa nchini Kuwait kwa miaka 36 sasa. Wasimamizi wa maonyesho hayo wanasema kuwa hiyo ni miongoni mwa njia bora zaidi za kueneza Uislamu duniani. 783047
captcha