IQNA

21:45 - May 02, 2011
Habari ID: 2116141

Waislamu watakiwa kusali kwa ajili ya kukombolewa al Aqsa

Kundi moja la wanaharakati wanaoshiriki katika mtandao wa kijamii wa Facebook limetoa wito kwa Waislamu wote wanaotumia mtandao huo kote duniani kuswali swala ya asubuhi ya Ijumaa ijayo na kuomba dua kwa ajili ya ukombozi wa Msikiti wa al Aqsa huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Wanahakati hao wa mtandao wa Facebook wamewataka watumiaji kuhudhuria kwa mamilioni kwenye mtandao huo Ijumaa asubuhi kwa ajili ya swala itakayoswaliwa kwa nia ya kukomboa msikiti huo mtakatifu.
Wanaharakati hao wanakadiria kwamba watu milioni 10 wtashiriki katika mpango huo.
Mmoja kati ya wahusika wa mpango huo wa swala ya kombozi wa Msikiti wa al Aqsa amesema mpango huo utatekelezwa duniani kote na amemuomba Mola Muweza kusaidia ukombozi wa Msikiti wa al Aqsa.
785045


captcha