IQNA

Insaiklopidia ya "Mwanamke na Utamaduni wa Kiislamu" yazinduliwa

21:47 - May 02, 2011
Habari ID: 2116142
Nakala ya intaneti ya insaiklopidia ya Mwanamke na Utamaduni wa Kiislamu imezinduliwa katika Kitivo cha Anthropolojia (elimu ya binadamu) cha Chuo Kikuu cha California.
Kituo cha Sociorel kimeripoti kuwa nakala asili ya insaiklopidia hiyo ilitayarishwa na zaidi ya wahakiki 900 kati ya mwaka 2003 hadi 2007 na inajumuisha makala 1246 katika juzuu 6.
Insaiklopidia hiyo ina makala kuhusu maisha ya wanawake wa Kiislamu katika nchi mbalimbali za Kiislamu na zisizokuwa za Kiislamu ambazo zimeandikwa na wahakiki wa vyuo vikuu kutoka pembe mbalimbali duniani.
Insaiklopidia hiyo pia ina makala kuhusu shughuli wa wanawake wa Kiislamu katika nyanja za siasa, uchumi, jamii, sheria, tiba na sayansi za kisasa. 785094

captcha