Amesema kuwa fikra ndizo zinazompa mwanadamu mbawa za kupaa katika anga za juu na kumfungulia milango. Amesisitiza kuwa fikra hubakia hai kwa kuandikwa na kuhifadhiwa na kwamba kitabu ndiyo njia na chombo bora zaidi cha kulinda na kudumisha fikra. Amesema mirathi kubwa zaidi ya mwanadamu inapatikana katika kurasa za vitabu na kwamba wenzo huo ndio muhimu zaidi katika kuunganisha nyoyo na fikra za wanadamu.
Rais Ahmadinejad amekosoa baadhi ya nchi za kibeberu zinazotumia bajeti ya dola bilioni 1200 kwa ajili ya silaha na kuziusia nchi hizo zilizodhidi ya binadamu kutumia sehemu moja tu ya fedha hizo kwa ajili ya kueneza fikra, elimu na maarifa duniani.
Amesema nchi za kibeberu zinataka kueneza amani na usalama kupitia njia ya vita na mabavu na kusisitiza kuwa lau kama sehemu moja ya fedha zinazotumiwa na madola ya kibeberu kwa ajili ya vita zingetumiwa kueneza kitabu na fikra, basi migogoro na mapigano yote duniani yangekoma. Amesisitiza kuwa anatarajia itawadia siku ambapo silaha zote zinazotumiwa kuua mwanadamu zitabadilika na kuwa kalamu.
Makampuni karibu elfu nne ya uchapishaji ya ndani ya nje ya nchi yanaonesha anwani zaidi ya laki nne za vitabu katika maonyesho ya sasa ya Tehran. Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu ya Tehran ambayo yanashirikisha mashirika ya uchapishaji kutoka nchi zaidi ya 67 duniani, ndio makubwa zaidi katika eneo la Mashariki ya Kati. 786183