IQNA

Kitabu kuhusu Vyuo vya Kitiba katika Ustaarbu wa Kiislamu

14:12 - May 08, 2011
Habari ID: 2118622
Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni ISESCO limechapisha kitabu kipya kwa lugha ya Kiarabu chenye anwani ya “Vyuo vya Kitiba katika Ustaarabu wa Kiislamu”.
Kwa mujibu wa wa tovuti ya ISESCO, kitabu hicho chenye kurasa 258 ni mjumuiko wa makala za kongamano kuhusu vyuo vya kitiba katika ustaarabu wa Kiislamu ambalo lilifanyika Tripoli, Libya mwaka 2006.
Kitabu hicho kinajumuisha makala 13 za utafiti pamoja na mapendekezo ya kongamano hilo. Dibaji ya kitabu hicho imeandikwa na Katibu Mkuu wa ISESCO Dkt. Abdulazizi Othman Altwaijri.
787705
captcha