Askari jeshi wa utawala wa Aal Khalifa wa Bahrain wakisaidiwa na askari vamizi wa Saudi Arabia nchini humo jana Jumamosi walifanya shambulio la kinyama dhidi ya nyumba ya Abdul Rauf as-Shayyib, Katibu Mkuu wa Harakati ya Uhuru ya Bahrain.
As-Shayyib ambaye pia ni msemaji wa Muungano wa Wanamapinduzi wa Februari 14 amesema kuwa askari hao walivamia nyumba yake katika mji mkuu Manama na pia shule ya chekechea iliyoko katika eneo jirani ambayo inasimamiwa na mke wake.
As-Shayyib amesema kuwa katika shambulio hilo lililotekelezwa na askari hao jana asubuhi, askari waliotajwa walimteka nyara mwana wa kiume wa kaka yake na kufanya upekuzi wa muda mrefu katika nyumba hiyo.
As-Shayyib ambaye ni mpinzani wa utawala dhalimu wa Bahrain anaishi mjini London Uingereza. 787898