Kwa mujibu wa taarifa wizara hiyo imesema kuwa mashindano haya yanaendeshwa kupitia Idara Kuu ya Masuala ya Qur'ani na ni sehemu ya juhudi zake za kukuza miradi inayolenga Qur'an'.
Wizara ilieleza kuwa lengo la mashindano haya ni “kuunga mkono wale waliodhamiria kujifunza Qur'ani na kuhamasisha ushiriki katika shughuli za Qur'ani kupitia majukwaa ya kidijitali.”
Ushiriki umewekewa kikomo kwa watu wanaohudhuria kwa ukawaida madarasa ya mtandaoni ya kujifunza Qur'an' yanayofanyika ndani ya Misri. Washiriki pia wanapaswa kufaulu mitihani ya awali ya kuhifadhi na kusoma ili waweze kuingia rasmi kwenye mashindano.
Malengo ya mashindano haya ni pamoja na kuwahamasisha vijana na wanafunzi kushiriki katika elimu ya Qur'an', kuunda mazingira salama na yenye msaada ya kujifunza mtandaoni, pamoja na kuwatambua wale walio na uwezo wa kipekee katika kuhifadhi na kusoma Qur'ani.
Mashindano haya yana makundi mbalimbali, yakiwemo kuhifadhi Qur'ani yote kwa tajwidi, nusu, robo tatu na robo moja ya Qur'ani kwa tajwidi, pamoja na usomaji wa Qur'ani na uwasilishaji wa tajwidi.
Mwishoni mwa mashindano, washiriki watakaoonyesha uwezo mzuri watatunukiwa vyeti rasmi vya kuhifadhi na kusoma Qur'ani pamoja na zawadi za fedha taslimu.
Wizara hiyo iliripoti kuwa hadi sasa jumla ya madarasa 96 ya mtandaoni ya kuhifadhi Qur'ani yamefanyika, na watu 1,776 wamehusika, takwimu ambazo zinaonyesha muitikio mkubwa kwa mpango huo.
3493839