Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, jumuiya hiyo ilimkemea Rais wa Marekani Donald Trump kwa kuvunja maadili ya kimataifa na kuidhalilisha imani ya Waislamu zaidi ya bilioni moja na nusu duniani kote.
Taarifa hiyo imeweka wazi kuwa matamshi hayo ya matusi ya kidhalimu ni ishara kuwa mapambano ya kihistoria dhidi ya dhulma yanaendelea. Wanaharaakti hao wamesema: “Hatua hii ya kiburi inatokana na jeuri, ujinga, na kushindwa kwa mikakati ya ubeberu wa kimataifa na uzayuni. Ni jaribio la mwisho la kuudhoofisha umoja wa Ummah wa Kiislamu na kuporomosha misingi yake ya kiroho na kisiasa.”
Taarifa hiyo imekumbusha onyo la Qur’an Tukufukwa wale wanaopinga mwongozo wa Mwenyezi Mungu, ikitaja aya kutoka Surah Aal Imran (3:21) na Surah Al-A’raf (7:150), zinazozungumzia upinzani uliowakumba manabii kama Nabii Musa (A.S).
“Hili si tusi tu kwa Marjaa wetu ya kidini, bali ni shambulizi dhidi ya utambulisho wa pamoja wa ulimwengu wa Kiislamu,” taarifa iliendelea. “Ni mwendelezo wa mbinu dhalimu zilizotumika na madikteta wa enzi zote.”
Jumuiya ya Wanaharakati wa Qur’an Iran imezitaka taasisi za Kiislamu, wasomi wa Kiislamu, mashirika ya kimataifa kama Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC), na mataifa yenye Waislamu wengi kulaani vikali dharau hiyo na kuhamasisha juhudi za kisiasa, kisheria, na kimtandao katika kutetea maadili ya Uislamu.
“Sauti za wanazuoni wetu na watu wenye fikra lazima ziwe za busara na ujasiri,” taarifa imehimiza, ikinukuu Surah Ash-Shu’ara (26:227):
“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.”
Aya hiyo inabashiri ushindi wa haki juu ya batili na kushindwa kwa madhalimu, taarifa inasisitiza.
“Kwa kutegemea ahadi hii ya Mwenyezi Mungu na tukihimizwa na historia yetu tukufu, Ummah wa Kiislamu utathibitisha tena kuwa hautasalimu amri kwa njama za maadui wake, bali utaendeleza njia ya muqawama na mwamko kwa heshima na mamlaka.”
Taarifa imemalizia kwa ahadi ya kupinga uonevu wowote, ikitangaza utayari wa “kuyatumia rasilimali zote, ndani ya Iran na duniani kote, kupambana na kushinda hawa mahasidi wenye nia mbaya.”
Katika matamshi yake ya chuki ya kawaida, Rais wa Marekani siku ya Ijumaa alitoa matusi mazito dhidi ya Ayatullah Ali Khamenei, akidai kuwa alikuwa amezuia jeshi la Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel kumuua.
3493670