IQNA

Mtazamo

Mikataba ya Abrahamu ya Trump Imeandikiwa Kushindwa: Mchambuzi

20:15 - July 09, 2025
Habari ID: 3480922
IQNA – Mkataba wa Abrahamu wa Trump (ujulikanao pia kama "UAbrahamu wa Trump"), ambao unalenga kudhoofisha dini na haki za kitaifa za Wapalestina, hauwezi kufikia malengo yake, kwa mujibu wa mchambuzi wa kisiasa kutoka Lebanon.

Mikataba hii, inayojulikana kama "Abraham Accords", ilikuwa ni mikataba ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya utawala wa Kizayuni (Israel) na baadhi ya nchi za Kiarabu, ikiwemo Falme za Kiarabu (UAE), Bahrain, Sudan, na Morocco, kwa msukumo na uungwaji mkono wa utawala wa Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump.

Mikhail Awad, mwandishi na mchambuzi kutoka Lebanon, kupitia Makala aliyoandikia  katika Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) , alieleza namna mikataba hii ilivyo chombo cha kuharibu maadili ya kidini na haki za kitaifa za Wapalestina. Anasema:

Trump si mtu wa dini, si wa kiitikadi wala wa mkakati wa kina bali ni mfanyabiashara wa mikataba. Dini si kipaumbele chake, faida binafsi ndiyo msingi wake. Mbinu zake zinategemea nguvu, vitisho na ukatili; ambavyo vinapingwa na dini zote za mbinguni na hata fikra za kidunia. Hakuna dini, tamko la haki za binadamu, wala taifa lililowahi kuhalalisha au kuunga mkono aina hii ya mikataba.

Katika muhula wake wa kwanza, Trump alikuja na mpango wa "Makubaliano ya Karne", ambao ulifeli vibaya. Katika muhula wake wa pili, alipendekeza kuigeuza Gaza kuwa "Riviera ya Mashariki ya Kati", wazo ambalo lilikataliwa na watu wa Gaza wanaopitia mauaji ya kila siku na mateso makubwa.

(Riviera ni neno la Kifaransa linalomaanisha ukanda wa pwani wenye mandhari ya kuvutia, hali ya hewa nzuri, hoteli za kifahari, na vivutio vya watalii. Riviera huko Ufaransa huwa ni vituo vya ufuska.)

Sasa, Trump anasukuma mpango mwingine kwa kivuli cha "UAbrahamu" na "Dini ya KiAbrahamu". Lengo lake si la kiroho wala kidini, bali ni kuunda upya dini na maadili yake ili yafae maslahi yake binafsi na mtazamo wake wa kimikataba.

Lakini dini za mbinguni na maadili yake vimejikita sana katika akili, tamaduni na staarabu za mataifa haviwezi kuuzwa wala kufanywa bidhaa ya kisiasa.

Malengo ya Mkataba wa Abrahamu ni Mawili:

Kwanza: Kudhoofisha dini kwa kuziunda upya ili ziendane na thamani za Trump na mataifa yenye nguvu yanayonyanyasa mataifa mengine. Mpango huu unapingana kabisa na mafundisho asili ya Nabii Ibrahim au Abrahamu (AS), aliyetetea ukweli, haki, na kupinga dhulma, uporaji na ukandamizaji wa haki za binadamu.

UAbrahamu wa Trump umetokana na ujinga na kisasi, ukienda kinyume kabisa na ujumbe halisi wa Nabii Ibrahim (AS). Unalenga kufuta historia, kupindua dini na manabii, na kurudisha jamii katika enzi za ujahili au ujinga uliokuwepo kabla ya mitume kuja kuwaongoza watu.

Dini ya Nabii Ibrahim na Uyahudi vilikuwepo kabla ya kuja kwa Kristo, lakini bado Wayahudi wanakataa Nabii Isa  au Yesu (AS). Hii ni katika hali ambayo, ukweli ni kuwa Isa alikuja na alifungua njia ya kuja kwa Nabii Muhammad (SAW).

Uyahudi uliweka misingi ya mahusiano ya kiroho kati ya mwanadamu na Muumba. Ukristo ulibeba Amri Kumi kama mwongozo wa maadili. Uislamu, kupitia Qur’an, uliweka misingi ya mwisho ya ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa wanadamu wote.

UAbrahamu wa Trump unalenga kuvunja haya yote, na kuruhusu vitendo vya dhuluma, unyang’anyi, ushahidi wa uongo, tamaa za wake wa ndugu, na hata mauaji kwa jina la dini, kama wafanyavyo Israel, Marekani, na vibaraka wao wa kisiasa na kijeshi.

Pili: Kuweka msingi wa kifikra na kiitikadi kwa miradi ya kufuta haki za kitaifa, kikabila, kidini, na kibinadamu za Wapalestina.

"UAbrahamu" huu uliojengwa juu ya upotoshaji wa dini, unaangamiza imani ya kweli na kutoa nyenzo kwa wafuasi wake kuifuta Kadhia ya Palestina,kwanza kwa nadharia, halafu kivitendo.

Lakini hali halisi si kama wanavyodhani. Kadhia ya Palestina si mzozo wa kidini au wa dini dhidi ya dini nyingine. Gaza imefichua uongo, madai ya kipropaganda, na njama zote.

Gaza ni ya Wapalestina, Waislamu, Masunni, walio karibu na Ikhwanul Muslimin, Mawahabi na Salafi, lakini bado wanachinjwa hadharani. Makundi yote ya Kiislamu ya kisiasa na kijeshi, yakiwemo Wahabi, Salafi, na Ikhwanul Muslimin, yameshiriki kwa njia moja au nyingine kuruhusu mauaji haya.

Nchi zinazoongozwa na tawala za Kiarabu na Kiislamu pia ni washirika wa maangamizi haya ya Gaza, uharibifu na uhamishaji wa Wapalestina.

Kinyume na madai ya kiitikadi, ni Wakristo, Wayahudi wasio Wazayuni na watu wa fikra huru duniani, hasa Ulaya na Marekani, wanaosimama na Gaza, wakiongoza maandamano, wakilipa gharama ya mshikamano, na kuonyesha ujasiri wa kweli.

Wakati huo huo, makundi ya Kiislamu ya kisiasa yamegeuka kuwa mawakala wa kawaida wanaosaidia mradi wa Kizayuni kwa "uhusiano wa kawaida".

Hitimisho:

Mikataba ya Abrahamu haiwezi kufanikisha malengo yake. Haiwezi kupotosha dini au kuzivunja. Labda itazaa dhehebu potofu kama ilivyo kawaida katika historia ya dini, lakini haiwezi kuharibu imani ya kweli, utambulisho wa kitaifa, wala haki.

Katika enzi ya akili mnemba, majaribio ya upotoshaji kama haya yanaweza kuongezeka kwa maelfu au hata mamilioni.

Hata hivyo, kuharibu haki za kitaifa si njia ya kuleta amani. Historia imethibitisha kuwa haki haiwezi kufutwa au kugawanywa, huweza tu kurejeshwa. Hili linabakia kweli kwa Palestina, kwa mujibu wa mabadiliko yote ya wakati.

Ni lazima kufichua na kupinga UAbrahamu huu bandia kwa njia zote. Tusidanganyike na maneno matamu au ahadi zisizo na dhamira.

Kama vile "Mpango wa Karne" ulivyoshindwa, na machakato wa 'kuwa na uhusiano wa kawaida na Israel ulivyoanguka', ndivyo pia "mahesabi ya UAbrahamu" nayo pia yatashindwa. Na muda upo mikononi mwa Mwenyezi Mungu na irada ya mataifa.

4292999

captcha