Kituo cha kwanza kabisa cha Kiislamu chenye msikiti, kituo cha Kiislamu na jumba la makumbusho kinajengwa katika mji mkuu wa Albania, Tirana kwa lengo la kuimarisha urafiki na uhusiano kati ya wafuasi wa dini mbalimbali.
Kituo hicho ambacho kinajengwa katika ardhi yenye ukubwa wa mita mraba 27 elfu, kitakuwa nembo ya uvumilivu wa kidini nchini Albania.
Kituo hicho kitakuwa kikipokea watu wote hata wasiokuwa Waislamu kwa shabaha ya kuwatambulisha dini tukufu ya Kiislamu.
Msikiti wa kituo hicho utakuwa na uwezo wa kupokea watu 1000 na utajengwa kwa njia ambayo nuru ya jua itakuwa ikimulika ndani yake katika kipindi chote cha siku.
Vilevile kitakuwa na bustani ya Qur'ani ambayo itajumuisha mimea yote iliyotajwa katika Qur'ani. 787753