Kwa mujibu wa tovuti ya Sociorel maudhui muhimu zilizojadiliwa katika toleo hilo la kwanza ni pamoja na mazungumzo ya tamaduni mbalimbali, changamoto za zama katika uwanja wa utafiti na mijadala pamoja na shughuli za umma. Gazeti hilo linalochapishwa kwa lugha ya Kiingereza litakuwa likijadili masuala ya historia na tamaduni tofauti kwa madhumuni ya kuwanufaisha watu bila malipo yoyote. Maudhui kama vile falsafa za mazungumzo baina ya dini, suala la taqrib au kukurubisha pamoja madhehebu ya Kiislamu katika mtazamo wa kijamii na mkutano wa Kiislamu nchini Ujerumani zimejadiliwa katika kurasa za mwanzo za jarida hilo. Jarida hilo la intaneti litakuwa likitoa mara mbili kwa mwaka utafiti mpya kuhusiana na suala la kukurubisha pamoja madhehebu ya Kiislamu. 788373