Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO itatoa msaada wa kifedha kwa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Niger ikiwa ni katika fremu ya shughuli zake za kufadhili miradi ya pamoja ya Kiislamu.
Kutoa misaada ya masomo kwa wanachuo, kudhamini walimu wa lugha ya Kiarabu na masomo ya Kiislamu, vikao mbalimbali vya kiutamaduni na kimafunzo na pia kutoa misaada ya masomo kwa walimu ili wapate masomo ya juu ni sehemu ya misaada ya shirika hilo kwa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Niger.
Kuanzishwa kitengo cha lugha ya Kiarabu katika chuo hicho ni jambo jingine linalofutiliwa na Isesco.
Jumuiya ya Isesco inatazamiwa kushiriki katika kikao cha tatu cha Baraza la Uongozi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Niger ambacho kimepangwa kufanyika hapo Jumatatu na Jumanne za tarehe 16 na 17 za mwezi huu wa Mei. Masuala mbalimbali yakiwemo ya kielimu, kifedha na pia mipango ijayo ya chuo hicho yatachunguzwa katika kikao hicho. 790332