IQNA

Mapambano dhidi ya ugaidi yawahusishe wote

10:44 - May 15, 2011
Habari ID: 2122044
Kongamano la Kimataifa la Muungano wa Dunia dhidi ya Ugaidi kwa ajili ya Amani Adilifu limeanza Tehran kwa wito wa kuwahusisha wote katika mapamabno dhidi ya ugaidi.
Akihutubia kikao cha ufunguzi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kuyakurubisha Madhehebu ya Kiislamu Ayatollah Mohammad Ali Taskhiri amesema hakuna nchi yoyote inayopaswa kuruhusiwa ‘kuwa hakimu na mtekelezaji sheria’ katika kadhia ya ugaidi duniani.
Amesema Muungano wa Dunia Dhidi ya Ugaidi kwa ajili ya Amani Adilifu unalenga kuondoa kizingiti kikubwa cha ugaidi na kufuatilia maadili ya mwanadamu.
Amesisitiza kuwa wanadamu wote wanapaswa kushirikiana katika kuimarisha amani.
Kongamano hilo la siku mbili lilianza Jumamosi mjini Tehran na linawaleta pamoja wasomi 100 wa kimataifa pamoja na wataalamu 300 kutoka Tehran. Washiriki wanajadili njia za kuondoa ugaidi duniani.


791442
captcha