IQNA

Malaysia yakabiliwa na uhaba wa walimu wa masomo ya Kiislamu

12:25 - May 15, 2011
Habari ID: 2122353
Abdallah Adam, Mkuu wa Elimu katika jimbo la Sarawak nchini Malaysia amesema kuwa jimbo hilo linakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu wa masomo ya Kiislamu.
Shirika la habari la Bernama limemnukuu Bwana Adam akisema kuwa walimu wa masomo ya Kiislamu wanapasa kuwa na maarifa na ujuzi wa kutosha katika uwanja huo kwa sababu wanapasa pia kuwafundisha wanafunzi matawi ya dini. Amesema kuwa licha ya Wizara ya Elimu ya Malaysia kufanya juhudi kubwa za kutayarisha walimu wa masomo hayo lakini idadi ya wanafunzi pia imeongezeka na hivyo kutotatuliwa tatizo hilo.
Kwa mujibu wa ripoti, kuna walimu wapatao 43,000 katika shule za jimbo hilo lakini wengi wao hawana ujuzi wowote wa kufundisha masomo ya Kiislamu. 791223
captcha