Mashindano hayo ya wanaume yatakuwa katika vitengo vya hifdhi na qiraa.
Washiriki 30 kutoka maeneo mbalimbali ya Zimbabwe watashiriki katika mashindano hayo yatakayofanyika Mei 22.
Lengo la mashindano hayo ya Qur'ani limetajwa kuwa ni kustawisha utamaduni wa Qur'ani na kuwahimiza vijana Waislamu kusoma Qur'ani.
Washindi watashiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qurani ambayo hufanyika katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kila mwaka.
792152