IQNA

Kikao cha 'Ukamilifu wa Uislamu' kufanyika Russia

12:12 - May 21, 2011
Habari ID: 2124932
Kikao cha 'Ukamilifu wa Uislamu' kimepangwa kufanyika nchini Russia mwezi ujao wa Juni.
Kikao hicho kinaandaliwa na Jumba la Monyesho ya Kale la Armitage katika mji wa St. Petersburg. Mikhail Bitroviski mkuu wa jumba hilo amesema maafisa wake wamekuwa wakijadiliana na wakuu wa vituo na taasisi za Kiislamu za Russia ili kuchunguza historia ya Kiislamu na sifa zake maalumu katika maeneo tofauti ya nchi hiyo. Amesema maonyesho maalumu kwa jina la 'Mashariki na Magharibi; Sanaa ya Ulimwengu wa Kiislamu' yatafanyika pambizoni mwa kikao hicho.
Akiashiria kwamba Uislamu ndiyo dini ya pili kwa ukubwa nchini Russia, Armitage amesema kuwa ukuaji na ukamilifu wa Uislamu katika vipindi tofauti vya utawala wa nchi hiyo utachunguzwa katika kikao kilichotajwa.
Waandaaji wa kikao hicho wanasema kitakuwa na nafasi muhimu katika kuwavutia vijana na kuwabainishia kwamba dini ya Uislamu ni dini ya amani na upendo isiyokuwa na uhusiano wowote na ugaidi, kama inavyodaiwa na maadui wake. 794077
captcha