Masomo hayo ambayo yamepangwa kufanyika kwa muda wa siku nne hadi Alkhamisi tarehe 26 Mei huko katika mji wa Frankfurt yanadhaminiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Nchi za Kiislamu ISESCO.
Masomo hayo yanaendeshwa kwa ushirikiano wa Taasisi ya Uchapishaji na Huduma za Masomo pamoja na Jumuiya ya Maulama na Wahubiri wa Ujerumani iliyo na makao makuu yake katika mji uliotajwa.
Walimu 25 wamealikwa kushiriki kwenye masomo hayo. Kupewa mafunzo walimu watakaokuwa na uwezo wa kusomesha masomo ya Kiislamu, kuwapa mbinu za dharura za malezi na mafunzo, kusasishwa mbinu za masomo ya Kiislamu na kuoanisha masomo ya Kiislamu na mazingira ya sasa ni miongoni mwa malengo ya kuandaliwa masomo hayo maalumu. 796171