Katika taarifa hiyo, Ekmeleddin Ihsanoglu Katibu Mkuu wa OIC amewataka viongozi wa serikali, makundi ya kijamii na makabila ya nchi hiyo kuwa na subira na kutojihusisha na vitendo vya ghasia dhidi ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo. Ametaka mgogoro wa nchi hiyo utatuliwe kwa njia ya amani kupitia mazungumzo kwa lengo la kurudisha utulivu na amani nchini. Ameunga mkono mpango wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi wa kutatua mgogoro huo na kusema kuwa utachangia pakubwa katika kukabidhiwa madaraka kwa amani kutoka kwa Rais Abdallah Swaleh, na kuyataka makundi yote husika kuukubali mpango huo ili kurudisha amani na umoja nchini humo.
Katika upande wa pili, katibu mkuu huyo wa OIC ameeleza kufuraishwa kwake na kufunguliwa kwa kivuko cha Rafah kuelekea Ukanda wa Gaza unaozingirwa na utawala haramu wa Israel. Kivuko hicho ni muhimu sana katika kuvukisha bidhaa muhimu za chakula na madawa kwa ajili ya kuwasaidia Wapalestina wanaozingirwa na Wazayuni wa Israel. 799046