Mkuu wa shirika hilo Muiz Shakshok amesema shirika lake halikubali uamuzi wa Mahakama ya Mwanzo iliyosisitiza juu ya udharura wa kuchujwa mitandao yote inayopingana na maadili na mafundisho ya Uislamu na tayari limeiandikia barua mahakama hiyo ikiitaka isimamishe utekelezaji wa hukumu yake.
Siku chache zilizopita Mahakama ya Mwanzo ya Tunisia ilitoa hukumu ikilitaka shirika linalotoa huduma za intaneti nchini humo kuchuja mitandao yote inayochapisha au kuandika mambo yanayopingana na maadili mema na thamani za Kiislamu. Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na taathira za mitandao hiyo michafu kwa fikra na muundo wa kijamii na kimalezi wa Tunisia.
Ripoti zinasema kuwa mitandao ya ufuska na mambo machafu imeenea mno nchini Tunisia baada ya mapinduzi ya kiraia yaliyomuondoa madarakani dikteta wa zamani wa nchi hiyo Bin Ali. 801724