Mkuu wa Baraza Kuu la Aalul Bait nchini Misri Sayyid Muhammad al Darini amesisitiza katika mkutano uliofanyika Cairo juu ya udharura wa kufunzwa fiqhi ya Ahlul Bait (as) sambamba na fiqhi za madhehebu nyingine za Kiislamu katika Chuo Kikuu cha al Azhar.
al Darini ameashiria kwamba vijana wa Misri wamenyimwa fusra ya kujifunza fiqhi ya Ahlul Bait (as) kwa miaka mingi na akaongeza kuwa kufunzwa fiqhi hiyo katika Chuo Kikuu cha al Azhar kutawapa vijana fursa ya kutambua fiqhi ya Waislamu wenzao wa madhehebu ya Shia.
Wanachama wa Baraza Kuu la Aalul Bait la Misri pia wamesisitiza juu ya udharura wa kukomeshwa harakati za kundi la Kiwahabi la masalafi na mipango yao inayozusha hitilafu na mifarakano. 804007