IQNA

IQNA kuanzisha kitengo cha habari za wenye ulemavu wa macho

13:59 - June 07, 2011
Habari ID: 2134126
Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani IQNA lenye makao yake nchini Iran linapanga kuanzisha kitengo maalumu cha wenye ulemavu wa macho.
Kitengo hichi kitaanzishwa kwa majaribio tarehe 13 Rajab (Juni 16) kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Ali bin Abi Twalib AS.
Hatua hii inalenga kuwawezesha wenye ulemavu wa macho kupata fursa ya kusoma Qur'ani na habari za Kiislamu kupitia intaneti.
IQNA kama shirika la kwanza na pekee la habari za Qur'ani duniani linalenga kuwa na viwango vya juu katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwawezesha watumiaji wote wa intaneti kupata habari za Qur'ani bila kizingiti.
Watu vipofu au wenye ulemavu wa macho wanahitajia programu maalumu kusoma kurasa za intaneti na hili linahitaji viwango maalumu. Shirika la Kimataifa la Habari za Qur'ani lina fahari kuwa la kwanza kuchukua hatua hii.
803952
captcha