Akizungumza hapo siku ya Jumanne katika makumbusho ya mwaka wa 22 ya kuaga dunia Imam Khomeini (MA), mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, Balozi Hassan Danaifar amesema kuwa tokea huko nyuma Jamhuri ya Kiislamu Iran imekuwa ikiunga mkono mpango huo na kusisitiza kwamba iko tayari kushirikiana na gavana wa mji wa Najaf ili kufanikisha jambo hilo. Amesema Iran iko tayari kutoa huduma zote kwa ajili ya kuhudumia mji mtakatifu wa Najaf ili kuarifishwa vyema mji huo mbele ya walimwengu.
balozi wa Iran nchini Iraq amesema Najaf ambako ndiko alikozikwa Imam Ali (as) ni kituo muhimu cha elimu ya Kiislamu ambacho kimekuwa kikilea na kutoa wanazuoni mashuhuri wa Kiislamu duniani. Mawaziri wa Utamaduni wa nchi za Kiislamu walikutana huko mjini Baku, mji mkuu wa Azerbaijan mwezi Agosti 2008 na kutangaza Najaf kuwa mji mkuu wa utamaduni wa ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2012. 805216