Kituo cha Islam Online kimeripoti kuwa katika mpango huo ambao utatoa changamoto dhidi ya hisia za chuki dhidi ya Uislamu katika jamii ya Marekani kutatarishwa mabango ya matangazo na kuwekwa katika maeneo mblimbali ya mji wa Houston.
Mkurugenzi Mtendaji wa CAIR Mustafa Carol amesema lengo la mpango huo uliopewa jina la Amani na Umoja ni kupambana na wimbi la chuki na hujuma dhidi ya Uislamu katika jimbo la Texas. Ameongeza kuwa katika mpango huo zinafanyika juhudi za kuzidisha uelewa na hali ya kufahamiana kati ya wafuasi wa dini mbalimbali na kudhihirisha mchango wa Waislamu katika jamii ya Marekani. 806661