IQNA

Sheikh wa al Azhar avitaka vyombo vya habari kueneza mafundisho sahihi ya Uislamu

16:11 - June 13, 2011
Habari ID: 2137627
Sheikh wa al Azhar Dakta Ahmad al Tayyib amevitaka vyombo vya habari kufanya jitihada za kueneza mafundisho sahihi na dini ya Kiislamu.
Ahmad al Tayyib ambaye jana alikuwa akihutubia kikao cha maulamaa, wanafikra na waandishi habari wa Misri mjini Cairo alivitaka vyombo vya habari kutangaza fikra za al Azhar na mitazamo ya wastani.
Vilevile Sheikh wa al Azhar na maulamaa waliohudhuria kikao hicho wamevitaka vyombo vya habari kueneza moyo wa kuvumiliana na mitazamo ya wastani na kujibu fatuwa zisizokuwa sahihi.
Kikao hicho ni katika ajenda ya al Azhar ya kuitisha mazungumzo kati ya wasomi na maulamaa wa Misri kwa ajili ya kufikia mtazamo mmoja kuhusu njia za ustawi na maendeleo ya Misri. 807853

captcha