Kikao hicho cha siku tatu kimefunguliwa kwa hotuba ya Mwenyekiti wa Baraza la Utendaji la ISESCO Abubakar Dukure.
Dukure amesema kuwa kikao cha sasa cha baraza hilo kinatathmini mafanikio na matunda ya ISESCO na mipango yake ya baadaye.
Amesisitiza pia juu ya udharura wa kufanyika marekebisho makubwa na ya kimsingi katika masuala ya malezi, elimu na utamaduni wa nchi wanachama wa ISESCO.
Vilevile Mkurugenzi Mkuu wa ISESCO Abdul Aziz al Tuwaijri ametoa ripoti kuhusu mafanikio ya jumuiya hiyo katika nyanja mbalimbali. al tuwaijri amesema ulimwengu wa Kiislamu unakabiliwa na kipindi nyeti ambacho kitakuwa na taathira mbaya katika masuala ya usalama na ustawi wa nchi za Kiislamu. 808651