Kwa mujibu wa tovuti ya ic-el semina hiyo itafanyika katika maktaba kuu ya kituo kilichotajwa kuanzia saa mbili usiku kwa wakati wa London kwa mnasaba wa maadhimisho ya kuzaliwa Imam Ali (as).
Uzawa, maisha, uadilifu wa Imam Ali na utawala wake ni miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa katika semina hiyo. Wasomi na wanafikra mashuhuri wa Kiislamu wamealikwa kuzungumza katika semina hiyo.
Kituo cha Kiislamu cha London pia kimepanga kufanya shehere maalumu ya kusherehekea siku ya kuzaliwa Imam Ali (as) hapo siku ya Alkhamisi tarehe 16 Juni ambayo inasadifiana na tarehe 13 Rajab. Wapenzi wa Ahlul Beit yaani Watu wa Nyumba ya Mtume Mtukufu (saw) wamealikwa kushiriki kwenye sherehe hiyo. 808382