Akibainisha zaidi suala hilo, waziri huyo amesema kuwa zama hizi ni zama za upashaji habari na vyombo vya habari na kwamba nchi za Kiislamu zinapasa kufanya juhudi za kuimarisha vyombo vya habari vya ulimwengu wa Kiislamu kwa kuviwezesha kunufaika na teknolojia ya kisasa kabisa katika uwanja huo. Firdous Ashiq amesema katika mazungumzo hayo kwamba nchi yake ina hamu kubwa ya kubadilishana wataalamu wa masuala ya habari na nchi nyinginezo za Kiislamu.
Tunakumbusha hapa kwamba duru ya nane ya Mawaziri wa Habari wa Nchi za Kiislamu ilifanyika yapata miaka mitatu iliyopita huko Rabat, mji mkuu wa Morocco. 809214