IQNA

13:57 - June 21, 2011
Habari ID: 2142029

Kazakhstan, mwenyeji wa kikao cha kimataifa cha hujuma ya propaganda chafu dhidi ya Uislamu

Kikao cha Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC cha kuchunguza hujuma za propaganda chafu za kuwatisha watu kuhusu dini ya Kiislamu katika jamii za Magharibi kitafanyika tarehe 28 Juni katika mji mkuu wa Kazakhstan, Astana.

Habari hiyo imetangazwa na Rais Nursultan Abishuly Nazarbayev wa Kazakhstan ambaye ameongeza kuwa kongamano hilo litafanyika sambamba na mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Kiislamu utakaoendelea kwa kipindi cha siku tatu.
Amesema kuwa kongamano hilo litafanyika kwa lengo la kuchunguza na kupasisha mpango wa kushirikiana na nchi za Magharibi katika juhudi kupambana na wimbi la propaganda chafu dhidi ya Uislamu.
Rais wa Kazakhstan amesema mkutano wa kupambana na propaganda chafu dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi utasisitiza juu ya udharura wa kushirikishwa Umoja wa Mataifa katika mipango ya kukabiliana na hujuma ya kuwatisha watu kuhusu dini ya Kiislamu.
Vilevile amezitaka nchi zote za Kiislamu wanachama wa OIC kufanya juhudi kubwa za kuonyesha taswira sahihi ya Uislamu na kuarifisha thamani zake kwa walimwengu. 812670
captcha