Athari na kazi za kaligrafia ya Kiislamu zinaonyeshwa katika maonyesho ya kaligrafia yaliyopewa jina la Rana Riyadh Ahmad, mchoraji mashuhuri wa Pakistan. Maonyesho hayo yanaendelea katika Jumba la Kitaifa la Sanaa ya Pakistan huko katika mji mkuu Islamabad.
Kwa mujibu wa tovuti ya Pak Observer, athari na kazi 32 za kaligrafia ya Kiislamu ambazo zinaarifisha turathi ya Kiislamu, zinaonyeshwa katika maonyesho hayo yaliyopangwa kuendelea hadi Jumapili tarehe 26 Juni.
Riyadh Ahmad kama tulivyoashria mwanzoni ni msanii mashuhuri wa Pakistan ambaye anatumia teknolojia ya kisasa katika uandishi wa Qur'ani na majina ya Mwenyezi Mungu katika sanaa ya maandishi ya mkono. 811948