IQNA

Mazishi ya Ustadh Shoaisha yafanyika baada ya sala ya Ijumaa Cairo

11:13 - June 25, 2011
Habari ID: 2143421
Mazishi ya karii mashuhuri wa Qur'ani nchini Misri, Sheikh Abolainain Shoaisha yamefanyika Ijumaa 24 mjini Cairo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA mjini Cairo Mahmud Jaber, Ustadh Shoaisha alilazwa hospitalini Cairo siku ya Jumatano na kuaga dunia Alkhamisi usiku.
Jaber ambaye ni mwanachama wa Baraza Kuu la Ahul Bayt AS nchini Misri ameongeza kuwa wataalamu wa ngazi za juu wa Qur'ani nchini humo pamoja na maulamaa kutoka nchi mbalimbali walihudhuria mazishi ya karii huyo maarufu wa Qur'ani.
Amesema kuwa wananchi wa Misri wapendao Qur'ani Tukufu wamesikitisha na kuaga dunia Ustadh Shoaisha ambaye alikuwa karii wa mwisho kutoka katika kundi la makarii bingwa wa zama za dhahabu za kiraa ya Qur'ani nchini Misri.
814172
captcha