IQNA

11:35 - June 25, 2011
Habari ID: 2143778

Serikali ya muda ya Tunisia yafanya juhudi za kuimarisha mfumo wa benki za Kiislamu

Beji Caid Essebsi, Waziri Mkuu mpya wa serikali ya mpito ya Tunisia amesisitiza juu ya umuhimu wa kuimarishwa mfumo wa benki za Kiislamu nchini humo.

Kwa mujibu wa tovuti ya businessnews Essebsi ambaye alikuwa akizungumza na Mahfoudh Baruni, mkuu wa Benki ya Az-Zeituna amesema kuwa serikali yake inaunga mkono kikamilifu juhudi za kuimarishwa mfumo wa benki za Kiislamu katika nchi hiyo. Baruni ameongeza kuwa katika mazungumzo yake na Essebsi wawili hao waliafikiana kunyanyua shughuli za benki ya az-Zeituna na kufikia kiwango cha kitaifa na kwamba benki hiyo iendeshe shughuli zake kwa msingi wa mfumo wa kifedha wa Kiislamu na sheria za Kiislamu.
Ameongeza kuwa masuala mengine yaliyojadiliwa ni kuhusiana na jinsi ya kuimarisha uhusiano wa benki hiyo na Benki ya Ustawi wa Kiislamu na kuarifishwa mfumo huo wa kifedha katika nchi nyinginezo.
Waziri Mkuu wa Tunisia pia alizungumza katika kikao hicho kuhusiana na mali za Zeinul Abedin bin Ali, rais wa zamani wa nchi hiyo aliyeng'olewa madarakani hivi karibuni na Watunisia na kulazimika kukimbilia nchini Saudi Arabia. 814373
captcha