IQNA

18:08 - June 29, 2011
Habari ID: 2146723

Kikao cha kila mwaka cha Jumuiya ya Vijana Waislamu chaanza leo Brussels

Kikao cha kila mwaka cha Jumuiya ya Vijana na Wanachuo Waislamu wa Ulaya kimeanza leo katika mji wa Brussels na kitaendelea hadi Jumatatu ijayo.

Kituo cha habari cha Saphirnews kimeripoti kuwa mamia ya vijana na wanachuo Waislamu wanachama wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ulaya na shakhsia wa Kiislamu kutoka nchi mbalimbali za bara hilo wanashiriki katika kikao hicho.
Jumuiya ya Vijana na Wanachuo Waislamu wa Ulaya imetangaza kuwa lengo la kikao hicho ni kuboresha hali ya kizazi kijacho cha Waislamu barani humo. Taarifa ya jumuiya hiyo imeongeza kuwa mkutano huo ni hatua muhimu katika juhudi za kuboresha hali ya kizazi kijacho cha Waislamu barani Ulaya na kusaidia viongozi wa kisiasa na kidini ili waweze kuchukua maamuzi bora na sahihi zaidi. 817560

captcha