IQNA

20:26 - July 02, 2011
Habari ID: 2147689

Kumbukumbu ya mwaka wa pili tangu kuuawa Shahidi wa Hijabu

Shughuli za mwaka wa pili wa kukumbuka mauaji ya "Shahidi wa Hijabu" Bi Marwa al Sharbini, mwanamke wa Kiislamu wa Misri zilifanyika jana katika mahakama ya mji wa Dresden nchini Ujerumani.

Shughuli hiyo imehudhuriwa na viongozi wa jimbo hilo akiwemo Meya wa mji wa Dresden, wawakilishi wa jumuiya za Kiislamu na taasisi zisizokuwa za Kiislamu za Ujerumani. Shughuli hizo imefanyika mahakamani alipouawa mwanamke huyo wa Kiislamu kwa sababu tu ya kuvaa vazi la hijabu.
Hiyo jana pia kulifunguliwa kituo cha utamaduni kilichopewa jina la Marwa al Sherbini katika mji wa Dresden katika kumbukumbu ya mwaka wa pili tangu auawe shahidi.
Wakati huo huo baraza la wafuasi wa dini za waliowachache nchini Ujerumani na Baraza la Uratibu la Waislamu wa Ujerumani zimetangaza kuwa propaganda chafu za kuwatisha watu kuhusu dini ya Kiislamu na vitendo vya kuvunjiwa heshima misikiti na Waislamu vimeongezeka mno nchini Ujerumani.
Tarehe Mosi Julai 2009 Daktari Marwa al Sherbini, mwanamke Muislamu wa Misri aliyekuwa na umri wa miaka 32 mkazi wa Ujerumani alishambuliwa na Mjerumani mmoja mwenye misimamo ya kufurutu mipaka kupigwa kisu mara kadhaa tumboni na kuuawa shahidi akiwa katika ukumbi wa mahakama ya mji wa Dresden. 818651

captcha