IQNA

Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani yaanza India

17:35 - July 04, 2011
Habari ID: 2148821
Mashindano ya kitaifa ya Qur'ani ya India yameanza Julai 4 katika Kituo cha Kiutamaduni cha Sunni katika mji wa Kolkata.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA Kusini mwa Asia, mashindano hayo ya siku mbili yatamalizika Julai 5.
Kituo cha Kiutamaduni cha Sunni hutoa mafunzo kwa mahufadh wa Qur'ani Tukufu kutoka maeneo mbalimbali ya India na kuwatayarisha kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ambayo hufanyika katika nchi kama vile Iran, Saudi Arabia, Bahrain, Misri na Dubai.
Wanaochukua nafasi ya kwanza hadi ya tatu katika mashindano hayo ya India hupewa zawadi ya Rupia elfu kumi kwa nafasi ya kwanza, elfu tano kwa nafasi ya pili na elfu tatu kwa nafasi ya tatu pamoja na nishani kwa kila moja.
819579
captcha