Gazeti la al Sharq la Qatar limeripoti kuwa mashindano hayo ya hifdhi ya Qur'ani na Hadithi ya Comoro yatasimamiwa na Wizara ya Mambo ya Masuala ya Kiislamu na Jumuiya ya Masuala ya Kheri ya Comoro.
Mwakilishi wa jumuiya ya RAF Muhammad Salah Ibrahim amesema kuwa mashindano hayo yatajumuisha hifdhi ya Qur'ani na Hadithi na maarifa ya maswahaba wa Mtume Muhammad (saw). Ameongeza kuwa mashindano hayo yatawashirikisha wanawake na wanaume.
Mwakilishi wa RAF amesema kuwa awamu ya awali ya mashindano hayo itafanyika mwezi Ramadhani mwaka huu katika makao ya Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Comoro.
Muhammad Saleh Ibrahim amesema sherehe za kufunga mahindano hayo zitahudhuriwa na Rais Ikililou Dhoinine wa Comoro. 820400