IQNA

Ottawa, mwenyeji wa tamasha ya pili ya Qur'ani Tukufu

17:32 - July 09, 2011
Habari ID: 2151352
Tamasha ya pili ya Qur'ani Tukufu itafanyika tarehe 7 Agosti mwaka huu katika mji wa Ottawa nchini Canada.
Tamasha hiyo itafanyika kwa mnasaba wa mwezi wa Ramadhani kwa lengo la kuwafungamanisha zaidi Waislamu na Qur'ani katika mwezi huo mtukufu na kuarifisha kazi za wasanii wa Kiislamu kuhusu Qur'ani.
Miongoni mwa ratiba za tamasha hiyo ni pamoja na kuonyesha nakala za kale za Qur'ani tukufu, michoro, kaligrafia ya Qur'ani, maonyesho ya filamu zinazohusiana na Qur'ani, kiraa ya kitabu hicho na kadhalika.
Katika siku mbili za tamasha hiyo pia kutafanyika mashindano ya Qur'ami ya watoto. 822112

captcha