IQNA

Qari wa Palestina auawa shahidi katika shambulizi la anga la Israel Gaza

17:33 - July 16, 2025
Habari ID: 3480954
IQNA – Msomaji wa Qur’ani wa Palestina na mwimbaji wa kaswida za Kiislamu amekufa shahidi katika shambulizi la hivi karibuni la anga lililofanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza.

Alaa Azzam aliuawa pamoja na wanafamilia wake wote baada ya nyumba yao iliyoko eneo la Tel al-Hawa, Gaza City, kushambuliwa na ndege za kivita za Israel.

Utawala wa Israel ulianzisha vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 2023.

Tangu wakati huo, takriban Wapalestina 58,000, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wameuawa, huku uharibifu mkubwa ukishuhudiwa katika eneo hilo la pwani.

Novemba iliyopita, Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ilitoa hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na aliyekuwa waziri wa vita  Yoav Gallant kwa tuhuma za uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu huko Gaza.

Aidha, Israeli inakabiliwa na kesi ya mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kutokana na vita vyake dhidi ya Gaza.

Ifuatayo ni sehemu ya usomaji wa Qur’ani uliofanywa na Alaa Azzam:

3493861

Habari zinazohusiana
captcha