IQNA

Warsha ya mtadanoni kujadili jinsi Iran ilivyojibu uchokozi wa Israel

17:19 - July 16, 2025
Habari ID: 3480952
IQNA – Shirika la Kimataifa la Habari za Qur’ani limeandaa warsha ya kimtandaoni (webinar) ya kimataifa iitwayo "Hadhi na Nguvu ya Iran; Ujumbe Zaidi ya Makombora" itakayofanyika mwishoni mwa wiki hii.

Mkutano huo utafanyika siku ya Jumamosi, ukihudhuriwa na Mkuu wa Akadamia Kitaifa cha Masuala ya Elimu, Utamaduni na Utafiti (ACECR) pamoja na wataalamu na wahadhiri kutoka vyuo vikuu mbalimbali duniani.

Mazungumzo ya warsha hii ya mtandaoni yataangazia jinsi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilivyolinda mamlaka na uhuru wake wa kiardhi wakati wa vita vya siku 12 vya uchokozi vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni mwezi uliopita.

Miongoni mwa mada zitakazojadiliwa ni:

  • "Ulinzi wa kihalali wa Iran katika mfumo wa sheria ya kimataifa","Operesheni Ahadi ya Kweli III na mabadiliko ya mlingano wa kimkakati wa eneo","Kuuwawa kwa wanasayansi; uvunjaji wa sheria ya kimataifa."

Mkuu wa ACECR, Profesa Ali Montazeri, atatoa hotuba yake kupitia studio ya Mobin ya IQNA jijini Tehran, huku wazungumzaji wengine wakichangia kwa njia ya video kutoka maeneo mbalimbali.

Wazungumzaji hao ni pamoja na:

  • Mwanazuoni kutoka Lebanon, Talal Atrisi, Daktari Danial Bin Mohd Yusof kutoka Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Kimataifa Malaysia (IIUM), Profesa Dina Sulaeman kutoka Chuo Kikuu cha Universitas Padjadjaran nchini Indonesia, Mchambuzi wa masuala ya Palestina, Iyad Abu Nasser.

Webinar hiyo itatangazwa moja kwa moja kupitia tovuti ya Aparat: www.aparat.com/iqnanews/live  na hotuba zote zilizotolewa zitapatikana katika tovuti rasmi ya IQNA.

Tarehe 13 Juni, utawala wa Israeli ulianzisha uchokozi dhidi ya Iran, lakini Iran ilijibu kwa nguvu kupitia mashambulizi ya makombora na droni dhidi ya maeneo ya Wapalestina yaliyokaliwa kwa nguvu, hali iliyoilazimisha Israeli kuomba kusitishwa kwa mapigano.

3493864

Habari zinazohusiana
Kishikizo: iran vita israel iqna
captcha