Kwa mujibu wa tovuti ya lermf, RMF imetoa taarifa na kusema mahesabu ya wataalamu Waislamu wanaofungamana na jukwaa hilo wamebaini kuwa siku ya kwanza ya mwezi Ramadhani wa mwaka huu wa 1432 Hijria itasadifiana na Agosti 1 mwaka 2011.
Taarifa hiyo imesema kuwa kwa mujibu wa mahesabu sahihi, hilali haitaweza kuonekana kabla ya Julai 31.
Baraza la Waislamu Ufaransa ambalo ndio taasisi rasmi ya mawasiliano kati ya Waislamu na serikali bado halijatangaza msimamo wake kuhusu siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Idadi ya Waislamu nchini Ufaransa ni karibu milioni 5 na hivyo kuifanya kuwa idadi kubwa zaidi ya Waislamu Ulaya Magharibi.
822382