IQNA

Mkutano wa Zaka wafanyika Kashmir

17:49 - July 11, 2011
Habari ID: 2152761
Mkutano wa Zaka ulifanyika jana katika mji wa Srinagar kwenye jimbo la Kashmir.
Mkutano huo umefanyika chini ya usimamizi wa Shirika la Misaada na Utafiti wa Kiislamu la IRRT na kuwashirikisha wasomi, maulamaa, waandishi na wanaharakati wa masuala ya kijamii.
Miongoni mwa masuala yaliyochunguzwa katika mkutano huo ni pamoja na maana ya Zaka katika Uislamu na umuhimu wa kutoa Zaka kama njia bora ya kuwasaidia wenye haja.
Washiriki katika mkutano huo wamesisitiza kuwa mbali na kutoa Zaka, wanaharakati wa masuala ya kijamii wanaweza kutoa huduma kwa wenye haja na kutenga wakati wao kwa ajili ya watoto yatima. 823650
captcha