IQNA

Kongamano la kimataifa la Ustaarabu wa Kiislamu kufanyika Malaysia

17:49 - July 11, 2011
Habari ID: 2152762
Kongamano la Kimataifa la "Ustaarabu wa Kiislamu na Utambulisho wa Melayu" limepangwa kufanyika nchini Malaysia tarehe 14 na 15 Julai katika jimbo la Malacca nchini Malaysia.
Kituo cha ICICMI kimeripoti kuwa kongamano hilo litafanyika kwa hima ya Kitengo cha Utafiti wa Kiislamu cha Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Malaysia, Taasisi ya Melayu na Ulimwengu wa Kiislamu na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC).
Kongamano hilo la kimataifa litajadali masuala matatu makuu mbayo ni "Ulimwengu wa Melayu kama Kituo Kikuu cha Kuhuisha Ustaarabu wa Kiislamu, Ustaarabu wa Kiislamu katika Mfumo wa Elimu wa Sasa, na Utambulisho wa Melayu katika Utandawazi.
Kongamano hilo la siku mbili litafanyika kwa lengo la kutayarisha fursa ya kufanyika uchunguzi wa kisayansi kuhusu ustaarabu wa Kiislamu ndani ya utambulisho wa Kimelayu. 823802

captcha