IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia kufunguliwa Jumamosi

18:12 - July 13, 2011
Habari ID: 2154222
Mashindano ya 53 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia yatafunguliwa rasmi Jumamosi ijayo katika sherehe itakayohudhuriwa na mfalme na nchi hiyo na mke wake katika mji mkuu wa Malaysia, Kuala Lumpur.
Shirika la habari la Malaysia Bernama limeripoti kuwa Jumuiya ya Ustawi wa Kiislamu ya nchi hiyo ambayo ndiyo inayosimamia mashindano hayo imetoa taarifa ikisema kuwa mashindano hayo yatawashirikisha makarii 81 kutoka nchi 50 duniani.
Taarifa hiyo imesema idadi ya washiriki katika mashindano ya mwaka huu ni kubwa zaidi ikilinganishwa na ya miaka miwili iliyopita. Imesema makarii wanaume katika mashindano hayo ni 50 na 31 ni wanawake.
Jumuiya ya Ustawi wa Kiislamu ya Malaysia imetangaza kuwa mashindano hayo yatafanyika kwa kipindi cha siku nane kwa kaulimbiu ya "Utambuzi wa Kina wa Umoja wa Umma wa Kiislamu".
Mashindano hayo yatatangazwa moja kwa moja katika televisheni ya Malaysia na kituo cha mtandano wa intaneti cha Jumuiya ya Ustawi wa Kiislamu ya nchi hiyo chenye anwani ya: www.islam.gov.my . 825212
captcha