IQNA

Mashindano ya Qur'ani Kufanyika Najaf

9:07 - July 14, 2011
Habari ID: 2154239
Mkuu wa Jumuiya ya Wasomaji na Wanaohifadhi Qur'ani katika mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq amesema mji huo utakuwa mwenyeji wa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani mwakani.
Sayyid Qasim Al Hulw amesema mashindano hayo ni kati ya shughuli za kuadhimisha kutajwa Najaf kama Mji Mkuu wa Kiutamaduni katika Ulimwengu wa Kiislamu mwaka 2012.
'Kutakuwa shughuli nyinginezo za kiutamaduni za Qur'ani mwakani' ameongeza.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi za Qur'ani inayofungamana na Kituo cha Utamaduni cha Safa amesema kuandaa mashindano ya kaligrafia ya Qur'ani ni kati ya ajenda za kituo hicho.
Amesema wataalamu wa Qur'ani wa Iran, Misri na Lebanon watatoa mapendekezo yao kuhusu mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ya Najaf.
824804


captcha