IQNA

Kazi za dijitali katika maonyesho ya Qur'ani Tehran

16:46 - July 18, 2011
Habari ID: 2155940
Mkurugenzi wa kitengo cha teknolojia ya dijitali katika Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani mjini Tehran amesema kazi 20,000 za dijitali zitawasilishwa katika maonyesho hayo.
Abuzar Khayyati amesema kuwa ukumbi wenye mita 2500 mraba umetengwa kwa ajili ya teknolojia ya dijitali katika maonyesho hayo ambapo taasisi 100 za Qur'ani zitashiriki.
"Sehemu iliyotengwa haitoshi kwa ajili ya taasisi za Qur'ani zinazoshiriki na hivyo kunapaswa kuchukuliwa hatua za kuwezesha taasisi nyingi zaidi kushiriki katika maonyesho haya ya kimataifa", ameongeza.
Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Qur'ani yataanza mwishoni mwa mwezi wa Shaaban hadi tarehe 15 ya mwezi ntukufu wa Ramadhani katika Ukumbi wa Sala wa Imam Khomeini mjini Tehran.
824677
captcha