IQNA

Taasisi ya Haram ya Imam Hussein AS kuandaa vikao vya Qur'ani Senegal

16:54 - July 18, 2011
Habari ID: 2155946
Darul Qur'an al Karim inayofungamana na Taasisi ya Haram ya Imam Hussein AS imetangaza kuwa itaandaa vikao vya kusoma Qur'ani Tukufu katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.
Kwa mujibu wa tovuti ya Noon, Taasisi ya Haram ya Imam Hussein AS imetiliana saini mapatano na Taasisi ya Utamaduni ya Kimataifa ya Al-Muzdaherah ya Senegal kuhusu ushirikiano katika uga wa Qur'ani.
Hassan al Mansuri anayesimamia Darul Qur'an al Karim Karbala amesema: "Makubaliano hayo yanahusu kuandaa vikao vya Qur'ani mjini Dakar na vilevile mafunzo ya Qur'ani kwa wanachuo wa Kiafrika".
Al Sharif Mohammad Ali Mkurugenzi wa Taasisi ya Utamaduni ya Kimataifa ya Al-Muzdaherah ya Senegal amesema makubaliano hayo yalitiwa saini kufuatia Tamasha ya 7 ya Kimataifa ya Machipuo ya Shahada iliyofanyika katika Haram ya Imam Hussein AS mjini Karbala.
Taasisi ya Utamaduni ya Kimataifa ya Al-Muzdaherah ina matawi 16 katika nchi kadhaa za magharibi mwa Afrika na inalenga kueneza mafundisho ya Ahul Bayt AS.
826168

captcha