Haya ni kwa mujibu wa afisa wa Wizara ya Elimu ya Iran Bi. Mardhiya Mesgarzadeh ambaye ameongeza kuwa lengo la somo hilo fupi ni kutoa mafunzo ya misingi ya Qur’ani kwa wanafunzi.
“Somo hilo litajumuisha pia kiraa ya Qur’ani Tukufu”, ameongeza.
Kwa mujibu wa mpango huo waalimu wa masomo yote yakiwemo hisabati, sana, Lugha ya Kifarsi n.k wataanza somo kwa kusoma aya chache za Qur’ani na kuelezea maana yake.
Amesema tayari warsha zimefanyika katika shule za upili ili kujadili njia za utekelezaji mpango huo.
827066