IQNA

Mwakilishi wa Iran ang'ara mashindano ya Qur'ani ya Malaysia

15:44 - July 19, 2011
Habari ID: 2156534
Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia Hamid Ridha Abbasi meng'ara katika siku ya tatu ya mashindano hayo yanayofanyika mjini Kuala Lumpur.
Ripota wa IQNA katika mashindano hayo amesema kiraa maridadi ya Hamiid Ridha Abbasi ya aya za suratul Anbiyaa imewavutia watu wengi na kushangiliwa na hadhirina katika ukumbi wa mshindano hayo.
Siku ya tatu ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Malaysia iliendelea jana kwa visomo vya washindani watano wa kiume na wanawake wane. Wasomaji hao walikuwa kutoka nchi za Iran Guinea Bissau, Syria, Iraq, Bosnia Herzegovina, Maldiv na Mali.
Wasomaji Qur'ani 81 wa kiume na makarii 50 wa kike wanashiriki katika mashindano hayo.
Mashindano hayo yatamalizika tarehe 23 Julai. 827812

captcha