Shirika la Kiislamu la Elimu, Sayansi na Utamaduni ISESCO limelaani vikali hatua ya vikosi vya wanamaji vya utawala haramu wa Israel kutumia mabavu katika kusimamisha na kuteka nyara meli ya Dignité-Alkarama iliyokuwa imebeba misaada kwa ajili ya ya raia wa Ukanda wa Ghaza.
Taarifa ya ISESCO imesema kitendo hicho cha Israel ni jinai na ugaidi. ISESCO imeongeza kuwa mzingiro wa Israel huko Ghaza ambao umewanyima mamilioni ya Wapalestina wakazi wa eneo hilo chakula, dawa, na umeme ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.
ISESCO imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuushinikiza utawala haramu wa Israel usitishe mzingiro wake dhidi ya Gaza na kuacha kufanya kigaidi dhidi ya watu wa Palestina.
828320