IQNA

Mji mtakatifu wa Najaf kufukizwa marashi ya Qur'ani

14:09 - July 20, 2011
Habari ID: 2157132
Mji mtakatifu wa Najaf nchini Iraq leo tarehe 20 Julai utafukizwa kwa marashi ya Qur'ani Tukufu kutokana na kiraa za wasomaji Qur'ani wa Kimataifa waliokwenda Iraq kwa mnasaba wa kusherehekea mpango wa kuchaguliwa Najaf kuwa mji mkuu wa ulimwengu wa Kiislamu katika mwaka 2012.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mpango wa Najaf, Mji Mkuu wa Kiutamaduni wa Ulimwengu wa Kiislamu 2012 Ali Mirza amesema vikao makhsusi vya kiraa ya Qur'ani vitafanyika katika miji ya Najaf, Kufa, Karbala na Kadhimain.
Ameongeza kuwa vikao hivyo vinafanyika kwa shabaha ya kustawisha zaidi utamaduni wa Qur'ani kati ya kizazi cha vijana na kutayarisha wasomaji watakaoshiriki katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani katika mji mtakatifu wa Najaf.
Amesema kuwa mbali na wasomaji Qur'ani bingwa wa Iraq, makarii 22 na majaji wa kimataifa wa Qur'ani kutoka nchi mbalimbali wanashiriki katika mahfali hiyo. 828385
captcha